SEKTA YA UTALII KUUZA SERA ZAKE WAKATI WA MASHINDANO YA MAGARI
Bodi ya utalii nchini imesema kuwa itatumia vyema fursa ya mashindano ya mbio za magari ya Safari Rally Duniani (WRC) yaliyopangwa kuanza Alhamisi, ili kutangaza nchi hii kama kivutio kikuu cha utalii wa michezo.
Bodi ya Utalii (KTB) imesema wageni zaidi ya 10,000 wanatarajiwa kuhudhuria mashindano hayo ya siku nne huko Naivasha, kilomita 90 kaskazini magharibi mwa mji mkuu, Nairobi.
Afisa mkuu mtendaji wa KTB, June Chepkemei, amesema bodi hiyo inatumia mashindano hayo kuiweka Kenya kama kivutio chenye uzoefu mwingi, ambako wageni wanaweza kujiburudisha kwa safari za pwani, shughuli za kiutamaduni, na michezo ya mbio za magari.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































