UPINZANI WATANGAZA KUIMULIKA SERIKALI
Viongozi wa muungano wa upinzani nchini wametangaza kuiweka serikali mbioni, kwa kuweka wazi kila jaribio la ufisadi kwa lengo la kuhakikisha uwajibikaji na utendakazi bora kwa wakenya.
Wakizungumza katika kaunti ya Kiambu, viongozi hao akiwemo Rigathi Gachagua wa DCP, Kalonzo Musyoka wa Wiper na Eugene Wamalwa wa DAP-K, wamekosoa mwenendo wa ubinafsishaji wa mashirika ya umma, wanaosema unalenga kuwafaidi maafisa wakuu serikalini.
Wamemtaka Rais kuhakikisha uzingatiaji wa utawala wa sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































