KIBET AONYA DHIDI YA SIASA ZA UKABILA
Msaidizi wa Rais, Farouk Kibet, ameongeza joto katika mjadala wa kisiasa huku akionya viongozi wanaochochea siasa za kikabila, akihimiza siasa zinazolenga umoja wa kitaifa, ukuaji wa uchumi na maendeleo jumuishi kwa Wakenya wote.
Akizungumza katika eneo la Chebarus, eneobunge la Cherangany, Kibet alisema eneo hilo lina nafasi kubwa ya kunufaika kupitia ushirikiano na serikali ya kitaifa badala ya siasa za upinzani.
Aidha, ametoa wito kwa jamii ya Mulembe kuungana ili kuharakisha maendeleo katika ukanda wa Magharibi, akisisitiza mshikamano kama nguzo ya mafanikio ya kijamii na kiuchumi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































