MIDEVA AWANIA KIATU CHA DHAHABU
Mshambuliaji wa Ulinzi Starlets, Elizabeth Mideva, ameonyesha dhamira ya dhati ya kunyakua tuzo ya mfungaji bora katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini.
Mideva, aliyewahi kusoma katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Bishop Njenga, aliibuka nyota mwishoni mwa wiki alipofunga mabao matatu katika ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya mabingwa wa zamani Vihiga Queens, ushindi uliosukuma timu yake hadi nafasi ya pili ikiwa na alama arobaini na saba.
Mabao hayo yamefikisha jumla yake kuwa kumi, mabao mawili nyuma ya kinara Margaret Kunihira wa Police Bullets, huku mwenzake Joy Oriyo akishika nafasi ya tatu kwa mabao tisa.
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































