#Local News

KALUMA: OMOLLO HAUHUSIKI KUZALISHA WAHUNI

Mbunge wa Homa Bay Mjini Peter Kaluma, amemtetea katibu mkuu katika wizara ya usalama wa kitaifa Raymond Omollo dhidi ya tuhuma za viongozi wa upinzani kwamba alihusika kupanga uvamizi dhidi ya seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi jijini Kisumu.

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na mbunge wa Embakasi East Babu Owino, wamehusisha uvamizi huo na Omollo, mbali na matukio mengine ya matumizi ya wahuni dhidi ya viongozi wa upinzani nchini.

Hata hivyo kupitia taarifa, Kaluma amesema Omollo analengwa na mashambulizi kutoka kwa viongozi hao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *