#Local News

ICHUNG’WAH AONYA KUINGILIWA KWA IEBC

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah ameonya wanasiasa dhidi ya kuingilia shughuli za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, huku viongozi wa Kenya Kwanza wakitaka tume hiyo ibaki huru.

Ichung’wah amewataka wanasiasa kuepuka kuingilia michakato ya IEBC na badala yake kuunga mkono utendaji huru wa tume hiyo katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2027.

Kauli hiyo inajiri huku mjadala ukizidi kuhusu uhuru wa IEBC na haja ya kuhakikisha maandalizi ya uchaguzi yanaendeshwa kwa uwazi, bila ushawishi wa kisiasa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

ICHUNG’WAH AONYA KUINGILIWA KWA IEBC

KESI YA REX MASAI YAINGIA HATUA YA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *