KESI YA REX MASAI YAINGIA HATUA YA MWISHO
Vikao vya kusikiliza kesi ya uchunguzi kuhusu mauaji ya Rex Masai, aliyepigwa risasi wakati wa maandamano ya Gen Z mwaka 2024, vimekamilika baada ya takriban miaka miwili, huku jumla ya mashahidi 30 wa upande wa mashtaka wakitoa ushahidi.
Mtaalamu wa uchunguzi wa kidijitali kutoka IPOA Joshua Mutua amethibitisha kuwa video za kamera za CCTV zilizowasilishwa kama ushahidi hazikufanyiwa mabadiliko yoyote, akisema zilikabidhiwa IPOA kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu.
Pande husika sasa zinatarajiwa kuwasilisha hoja zao kwa maandishi mbele ya Hakimu Geoffrey Onsarigo, kabla ya mahakama kutoa uamuzi kuhusu uchunguzi huo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































