#Local News

NYORO AISUTA SERIKALI KUFUATIA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA

Kiongozi wa PPK na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ameongeza shinikizo kwa Rais William Ruto kuhusu matumizi ya fedha za umma, akitaka uwajibikaji zaidi katika matumizi ya serikali.

Akizungumza katika makao makuu ya chama hicho Nairobi, Nyoro ameikosoa serikali kwa kile anachodai ni matumizi ya kupita kiasi huku huduma muhimu zikikosa rasilimali, na kuhoji urithi ambao Rais Ruto anataka kuacha kwa taifa.

Nyoro pia ametaka mikutano ya kisiasa ilindwe kote nchini, akisema ongezeko la visa vya vurugu katika mikutano ya hadhara linatishia haki za kisiasa na utulivu wa taifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *