#Football #Sports

KIBWAGE ALAUMU KUCHELEWA KWA LIGI BAADA YA GOR MAHIA KUFUNGWA NA PYRAMIDS

Beki wa Gor Mahia Mike Kibwage amesema kuchelewa kuanza kwa Ligi Kuu ya FKF kulichangia kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Pyramids FC katika mechi ya kwanza ya Gor Mahia ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kibwage amesema tofauti ya viwango vya utimamu wa mwili kati ya Gor Mahia na wapinzani wao ilikuwa miongoni mwa sababu za matokeo hayo, huku timu hiyo ikiwa bado haijapata mechi za kutosha za ushindani.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kibwage pia ametaja makosa madogo katika mchezo huo kuwa sehemu ya kilichoifanya Gor Mahia kushindwa kuzuia Pyramids, licha ya kucheza mbele ya mashabiki wake katika Uwanja wa Nyayo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *