#Local News

RUTO AAGIZA MADENI YA KAUNTI YALIPWE KWA HARAKA

Rais William Ruto amemuagiza Mdhibiti wa Bajeti pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuharakisha uhakiki wa madeni yanayodaiwa na kaunti, akisema kucheleweshwa kwa malipo kunawaumiza wasambazaji wa huduma na kudhoofisha uchumi.

Ruto amesema kuchelewa kuwalipa watoa zabuni na watoa huduma kunapunguza matumizi ya fedha katika kaunti na kuathiri mzunguko wa fedha, akisisitiza haja ya kushughulikia madeni hayo kwa haraka.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *