ELIMU BORA YATAKA SERIKALI KUWAJAZIA PENGO LA UFADHILI WANAFUNZI WAPYA
Kikundi cha Elimu Bora Working Group kinasema maelfu ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliojiunga na vyuo vikuu Septemba bado hawajapata ufadhili wa HELB wala ufadhili wa masomo, huku kukiwa na sintofahamu kuhusu nani atalipia karo yao.
Muungano huo sasa unaitaka serikali kutoa fedha za muda kwa wanafunzi hao ili waweze kuendelea na masomo wakati wakisubiri uamuzi kuhusu mfumo wao wa ufadhili.
Wamesema hali hiyo imewaacha wanafunzi wengi katika sintofahamu kuhusu mustakabali wao wa masomo, huku wakitaka serikali kuchukua hatua za haraka kuhakikisha masomo yao hayaathiriki.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































