RUKU AHAKIKISHA SERIKALI IMEJIANDAA KUKABILI MVUA ZA EL NINO
Waziri wa Mipango Maalum Geoffrey Ruku amewahakikishia Wakenya kuwa serikali inaweka mikakati ya kupunguza athari za mvua za El Nino zinazotarajiwa.
Ruku amesema serikali inashirikiana na washirika pamoja na wadau mbalimbali kuweka hatua za kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.
Amesema hatua hizo zinalenga kulinda maisha ya wananchi na kupunguza madhara yanayoweza kutokea kutokana na mvua hizo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































