WATU WAWILI WAFARIKI BAADA YA BASI KUGONGANA NA LORI KWENYE BARABARA YA MOMBASA – NAIROBI
Watu wawili wamefariki na wengine kujeruhiwa baada ya basi la Dreamline kugongana na lori katika eneo la Mgalaani kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi.
Ajali hiyo imesababisha hofu miongoni mwa wasafiri huku majeruhi wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo pamoja na mazingira yaliyopelekea magari hayo kugongana.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































