KENYA YAIMARISHA MAANDALIZI YA EL NINO
Kenya inaendelea kuimarisha maandalizi ya majanga kupitia mpango unaotumia utabiri wa hali ya hewa kuchochea hatua za mapema kabla ya majanga kutokea.
Mpango huo unalenga kulinda maisha na mali kwa kutoa msaada mapema kabla ya hali kama ukame na mafuriko kuongezeka na kuwa dharura.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imeeleza utabiri wa mvua unaotarajiwa katika kipindi cha El Nino, huku hatua za mapema zikilenga kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































