OMANYALA AANZISHA KLABU MPYA YA MBIO KITALE
Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala ameendeleza mpango wake wa kukuza vipaji vya mbio za kasi katika jamii kwa kuzindua klabu nyingine ya Omanyala Sprints katika Shule ya Kitaifa ya Wavulana ya St Joseph’s Kitale.
Uzinduzi huo ni sehemu ya juhudi za Omanyala kuanzisha programu za mbio za kasi shuleni na kuwapa wanariadha chipukizi njia ya kukuza vipaji vyao kutoka utotoni hadi kufikia mashindano ya kiwango cha juu.
Klabu hiyo ya Kitale imezinduliwa muda mfupi baada ya Omanyala kuanzisha klabu kama hiyo katika shule yake ya zamani ya Friends School Kamusinga, huku akiendelea na ziara yake ya kutembelea shule za Magharibi mwa Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































