#Local News

WAFANYAKAZI WA SUKARI WATISHIA KUGOMA KUDAI MILIONI 2.7

Chama cha Wafanyakazi wa Mashamba ya Miwa na Sekta Shirikishi kimetishia kusitisha uzalishaji wa sukari kuanzia Alhamisi ili kushinikiza kulipwa kwa mishahara ya malimbikizo yenye thamani ya shilingi bilioni 2.7.

Katibu Mkuu wa chama hicho Francis Wangara amewataka wamiliki wa viwanda kusitisha shughuli kwa muda ili kujikinga na hasara zinazoweza kusababishwa na mgomo wa wafanyakazi.

Serikali ilikuwa imeahidi kulipa hadi shilingi bilioni 5.6 za malimbikizo yanayodaiwa na wadau wa sekta ya sukari baada ya viwanda vya sukari vinavyomilikiwa na umma kukodishwa mwaka 2025.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *