RUTO AAHIDI KUTATUA MALALAMISHI YA ARDHI YA MRADI WA DANGOTE
Rais William Ruto ameahidi kuwa malalamiko ya wakazi wa Lamu kuhusu kipande cha ardhi cha zaidi ya ekari elfu saba kinacholengwa kujengwa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote yatashughulikiwa kwa haki.
Ruto amesema mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni mbili utakamilika ndani ya miaka mitatu na kutoa ajira zaidi ya elfu 60 nchini, huku akisema wakazi wa Lamu na Wakenya kwa ujumla watanufaika.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi pamoja na mfanyabiashara Aliko Dangote, Ruto na Dangote wamesema watakabiliana moja kwa moja na yeyote atakayejitokeza kujaribu kuvuruga utekelezaji wa mradi huo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































