#Football #Sports

SHARKS NA MOMBASA UNITED ZAKUTANA KUPIGANIA NAFASI LIGI KUU

Kariobangi Sharks na Mombasa United zinaanza leo mchuano wa mchujo wa kupanda na kushuka daraja katika Ligi Kuu ya SportPesa, kwa mchezo wa kwanza utakaochezwa Mbaraki Sports Club.

Mshindi kwa jumla ya michezo miwili atapata nafasi ya 18 na ya mwisho katika Ligi Kuu ya SportPesa, huku atakayeshindwa akishuka hadi Ligi ya Taifa ya Daraja la Kwanza msimu ujao.

Sharks iliyomaliza mkiani mwa timu 18 za ligi kuu inalenga kusalia katika daraja hilo dhidi ya Mombasa United iliyomaliza ya tatu katika Ligi ya Taifa, huku kocha William Muluya akiwaomba wachezaji kuacha mzozo wa nje ya uwanja na kulenga ushindi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *