MAAFISA WA ZAMANI WA UMMA WAMESHTAKIWA KWA KOSA LA KUTUMIA VYETI BANDIA
Maafisa wawili wa zamani wa umma wamefikishwa katika Mahakama ya Kupambana na Ufisadi ya Milimani, wakikabiliwa na tuhuma za kutumia vyeti bandia vya masomo kupata ajira na fedha za umma. Kenneth Mwiti Kiogora na Daniel Mukoya Olando walikamatwa Jumatano na kufikishwa mahakamani Alhamisi, ambapo walikana mashtaka dhidi yao
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Mwiti, aliyekuwa Karani Msaidizi wa Pili katika Bunge la Kaunti ya Kiambu, anatuhumiwa kughushi cheti cha KCSE na kukiwasilisha kama cheti halali kilichotolewa na Baraza la Kitaifa la Mitihani, KNEC. Kesi hiyo inaendelea mahakamani.
Imetayarishwa na Jesac Angeyo
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































