WABUNGE WAKOSOA GHARAMA KUBWA ZA UENDESHAJI WA UCHAGUZI
Gharama kubwa za kuendesha uchaguzi mkuu nchini zimeibua mjadala mkali Bungeni, huku wabunge wakianza kuchambua Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi wa 2024.
Wabunge wamehoji sababu zinazofanya Kenya kuwa miongoni mwa nchi zinazotumia fedha nyingi katika kuendesha uchaguzi, hasa katika maandalizi na usafirishaji wa vifaa vya uchaguzi.
Baadhi ya wabunge wamehusisha gharama hizo na ukosefu wa imani ya kisiasa, wakisema kutokuaminiana miongoni mwa wanasiasa huchangia kuongezeka kwa mahitaji ya kiusalama na kiutendaji katika uchaguzi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































