#uncategorized

RUTO AMPINGA SIFUNA KUHUSU TOZO YA NYUMBA

Rais William Ruto amemkosoa seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, kuhusu pendekezo la kufutilia mbali tozo ya nyumba za gharama nafuu, akionya kuwa hatua hiyo inaweza kusababisha kupotea kwa maelfu ya nafasi za kazi.

Ruto pia amewataka wafuasi wake katika eneo la North Rift kubadilisha kauli za kumuunga mkono kwa muhula wa pili kuwa kura halisi wakati wa uchaguzi.

Rais aliyasema hayo siku ya pili ya ziara yake katika kaunti za Elgeyo Marakwet na Baringo, akiendelea kutetea mpango wa serikali wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *