RAIS AMEENDELEZA UKOSOAJI WAKE DHIDI YA TEP
Rais William Ruto ameendeleza ukosoaji wake dhidi ya kiongozi wa chama cha The Equitable Party, TEP, ambaye pia ni Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, akidai kuwa chama hicho hakina ajenda ya kuwanufaisha Wakenya.
Ruto amesema chama hicho, kilichozinduliwa siku chache zilizopita, kinapotosha wananchi badala ya kutoa suluhu kwa changamoto zinazowakabili.
Rais Ruto ametoa matamshi hayo akiwa katika ziara ya maendeleo katika kaunti za West Pokot na Trans Nzoia, huku mvutano wa kisiasa ukiendelea kushuhudiwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































