#Local News

BUNGE LATAKA SERIKALI KUMALIZA MGOMO WA WAHADHIRI

Bunge la Kitaifa limetoa wito kwa serikali kuingilia kati haraka na kumaliza mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma unaoendelea kuvuruga masomo.

Akifika mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Umma, Katibu Mkuu katika Wizara ya Elimu anayesimamia elimu ya juu, Beatrice Inyangala, amesema wizara inaendelea kufanya mazungumzo na wadau kutafuta suluhu ya mzozo huo.

Bunge linataka hatua za haraka zichukuliwe ili kurejesha masomo vyuoni na kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo yao bila usumbufu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *