#Local News

NYORO AIBUA MASWALI KUHUSU HISA ZA KENYA PIPELINE

Mbunge wa Kiharu na kiongozi wa People’s Party of Kenya, Ndindi Nyoro, amedai kuwa ununuzi wa takriban robo ya hisa za kampuni ya Kenya Pipeline ni mwanzo wa mpango wa bilionea wa Nigeria Aliko Dangote na Rais William Ruto kutwaa udhibiti wa kampuni hiyo ya umma.

Nyoro pia amemshutumu Rais Ruto kwa kuingilia mchakato wa uuzaji na ununuzi wa hisa za Kenya Pipeline kupitia mashirika ya serikali, akidai hatua hiyo ilinufaisha Dangote.

Hata hivyo, madai hayo yametolewa na Nyoro huku kukiwa na maswali kuhusu umiliki wa kampuni hiyo muhimu ya usambazaji wa mafuta nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *