#Local News

WAZIRI DUALE AMEAHIDI KUKABILIANA NA UFISADI UNAOHUSIANA NA FEDHA ZA EBOLA

Waziri wa Afya Aden Duale ameahidi kuchukua hatua za kuziba mianya yote ya ufisadi katika matumizi ya fedha zilizotengwa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini.

Amesema wizara yake itaimarisha usimamizi wa fedha hizo ili kuhakikisha zinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa, yakiwemo kuzuia maambukizi na kuimarisha huduma za afya.

Duale amesema hatua hizo zinalenga kuzuia kujirudia kwa changamoto zilizoshuhudiwa wakati wa janga la COVID-19, ambapo kulikuwa na madai ya ubadhirifu wa fedha zilizotengwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

WAZIRI DUALE AMEAHIDI KUKABILIANA NA UFISADI UNAOHUSIANA NA FEDHA ZA EBOLA

EPL: CHELSEA vs TOTTENHAM

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *