#Athletics #Sports

KIPTUM NA KANDIE WATWAA TAJI LA STANCHART MARATHON

Abraham Kiptum na Mercy Kandie Rotich wametwaa mataji ya mbio za kilomita 42 katika mashindano ya mwaka 2026 ya Standard Chartered Nairobi Marathon yaliyofanyika jijini Nairobi.

Kiptum alimaliza mbio za wanaume kwa saa mbili, dakika kumi na sekunde 35, huku Kandie akitwaa taji la wanawake baada ya kutumia saa mbili, dakika 31 na sekunde 25.

Wanariadha hao kila mmoja amejishindia kitita cha shilingi milioni mbili kwa ushindi wao katika mashindano yaliyowakutanisha wanariadha mashuhuri, wakimbiaji wa burudani, familia na washiriki kutoka mashirika mbalimbali.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *