#Football #Sports

MANCHESTER UNITED YACHAPWA 3-0 NA BOURNEMOUTH

Manchester United imezidi kuzama kwenye hali ngumu baada ya kupokea kichapo cha mabao matatu kwa bila nyumbani dhidi ya Bournemouth, matokeo yaliyoibua mashaka kuhusu mustakabali wa kocha Michael Carrick.

Uamuzi wa Carrick kumweka benchi nahodha Bruno Fernandes haukuzaa matunda, huku United ikifikisha mechi nane mfululizo bila ushindi na kushuka hadi nafasi ya 16 kwenye jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza, ikiwa na tofauti ya pointi moja pekee kutoka eneo la kushushwa daraja.

Bournemouth ilipata mabao kupitia Rayan, Marcus Tavernier na Evanilson, na kuichapa United kwa mabao matatu kwa bila katika uwanja wa Old Trafford kwa mara ya tatu ndani ya misimu minne.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *