#Local News

MUDAVADI: KENYA HAIVUNJI UHUSIANO NA WASHIRIKA

Mkuu wa Baraza la Mawaziri, Musalia Mudavadi, amesema Kenya itaendelea kushirikiana na mataifa ya kigeni huku ikiweka mbele maslahi ya taifa na uwekezaji wa kimkakati.

Mudavadi amesisitiza kuwa Kenya haina mpango wa kukatiza uhusiano na washirika wake wa jadi, wakiwemo mataifa ya Ulaya, Amerika na Mashariki ya Mbali.

Amesema ushirikiano huo utaendelea kuchangia maendeleo ya Kenya na bara la Afrika, huku taifa likilinda maslahi yake ya kiuchumi na kimkakati.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *