#Football #Sports

MAN CITY WALENGA KUPUNGUZA MWANYA DHIDI YA ARSENAL

Manchester City wana fursa ya kupunguza mwanya wa pointi kati yao na viongozi wa ligi ya EPL Arsenal hadi pointi 3 hapo kesho watakapoialika Fulham kabla ya Arsenal kufunga safari kucheza na Brentford walio katika fomu nzuri baadaye Alhamisi.

The Gunners wanasalia katika nafasi nzuri ya kunyakua taji la EPL baad aya kusubiri kwa zaidi ya miaka 22, ila ushindi wa City dhidi ya Liverpool Jumapili iliyopita huenda ukaashiria mwamko mpya kwa vijana hao wa Pep Guardiola, na mtelezo wa Arsenal huenda ukawafanya wakasubiri kwa miaka zaidi kabla yak una taji hilo.

Kichapo cha Liverpool kiliwavurugia mipango yao ya kushirikia dimba la klabu bngwa Ulaya, wanapojiandaa dhidi ya safari ngumu ya Stadium of Light kumenyana na Sunderland.

Na licha ya kufuzu awamu ya mwondoano ya dimba la klabu bingwa bara Ulaya, Newcastle na Tottenham wanajipata katika hali ngumu nyumbani, hali inayoibua maswali kuhusu mustakabali wa makocha Eddie Howe na Thomas Frank mtawalia.

Mechi za EPL zikiingia wiki ya 26 kuanzia leo usiku, swali sasa ni iwapo Manchester City wataendeleza mchezo mzuri walioonyesha dhidi ya Liverpool, na iwapo Arsenal wako tayari kuhimili shinikizo.

City wana mazoea ya kumaliza kwa gia ya juu katika ubingwa wa misimu 6 chini ya Guardiola, ila safari yao ingetamatika iwapo wangepoteza dhidi ya Liverpool wikendi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAN CITY WALENGA KUPUNGUZA MWANYA DHIDI YA ARSENAL

RONALDO ATAMATISHA MGOMO WAKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *