#uncategorized

KENYATTA UNIVERSITY WANYAKUA TAJI LA KUSF

Kenyatta University wamejinyakulia taji la soka la wanawake la Kenya Universities Sports Federation (KUSF) wakati wa mashindano ya International Women’s Day yaliyofanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha Taita Taveta mjini Voi.

Kenyatta University waliwashinda University of Eldoret mabao 2–0 katika fainali na kumaliza mashindano ya siku tatu bila kupoteza mchezo.

Mabao ya Sheila Juma na Hope Wandera katika kila kipindi yaliihakikishia KU ushindi huo na kurejesha taji hilo baada ya mwaka jana kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Masinde Muliro University.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *