RUTO, WABUNGE WA ODM NA UDA KUPOKEZWA RIPOTI
Kamati inayosimamia utekelezaji wa mkataba uliotiwa saini na kinara mwanzilishi wa ODM marehemu Raila Odinga na Rais William Ruto kuhusu ushirikiano wa chama hicho na UDA, pamoja na ripoti ya mazungumzo ya kitaifa, NADCO, imeratibiwa kuwasilisha ripoti yake hii leo.
Mwishoni mwa wiki jana, kamati hiyo maarufu kama Coin10, ilitangaza kukamilisha ripoti yake inapojiandaa kuiwasilisha kwa Rais William Ruto na wabunge kutoka vyama hivyo, Rais akisema yuko tayari kuwaeleza wakenya kuhusu hatua zilizopigwa tangu ushirikiano huo.
Hata hivyo, gavana wa Siaya James Orengo, amesisitiza kuwa ajenda 10 hazijatekelezwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































