DCP YAPANDA KWA UMAARUFU, UDA NA ODM KWENYE MTEREMKO
Uungwaji mkono wa Chama cha DCP chake aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua umeongezeka kutoka asilimia 6 mwezi Novemba mwaka jana hadi asilimia 16 mwezi Mei mwaka huu.
Hii ni kulingana na utafiti wa kampuni ya TIFA ikionyesha jinsi ambavyo chama hicho kimekuwa kwa kasi zaidi.
Utafiti huo pia unaonyesha kupungua kwa umaarufu wa vyama vya UDA na ODM, huku uungwaji mkono wa ODM ukishuka kutoka asilimia 32 hadi 18 na UDA kutoka asilimia 38 hadi 17.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































