#Local News

KALONZO AONDOA UWEZEKANO WA KUUNGANA NA RUTO

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amekataa uwezekano wowote wa kuungana na Rais William Ruto au kuingia katika makubaliano ya kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Akizungumza katika kaunti ya Machakos, Kalonzo aliikosoa serikali ya Kenya Kwanza, akiitaja kuwa fisadi na yenye kupotosha.

Kiongozi huyo wa upinzani amemtaka Rais Ruto kukabiliana naye moja kwa moja katika uchaguzi mkuu ujao.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *