NGOGOYO AMKOSOA SAKAJA KWA UONGOZI NAIROBI
Mbunge wa Kajiado Kaskazini Onesmus Ngogoyo amemkosoa Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, akidai utendakazi wake umedorora na kuifanya kaunti hiyo kukumbwa na changamoto za usafi na miundombinu.
Ngogoyo amesema barabara za kaunti zimeharibika huku madiwani wakiendelea kuibua malalamishi kuhusu uongozi, akimtuhumu Sakaja kwa kutofika ofisini na kuhudhuria mikutano.
Matamshi hayo yanajiri kufuatia hatua ya Sakaja kuondoka chama cha UDA na kujiunga na ODM, huku Ngogoyo akihoji rekodi yake ya uongozi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































