MALALAH APENDEKEZA SIFUNA NA GACHAGUA KWA TIKETI YA 2027
Naibu kiongozi wa chama cha DCP Cleophas Malalah amependekeza seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kuungana katika tiketi ya urais ya upinzani kukabiliana na Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027
Malalah anamtaka Sifuna kupeperusha bendera ya urais huku Gachagua akiwa mgombea mwenza, akisema muungano huo utaunganisha uongozi wa vijana na uzoefu wa kisiasa
Amesema Kenya inaweza kunufaika na mchanganyiko wa mawazo mapya na uzoefu katika uongozi wa nchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































