#Football #Sports

CARRICK APINGA UVUMI WA KUFUTWA MANCHESTER UNITED

Kocha wa Manchester United Michael Carrick amepuuzilia mbali madai kuwa amebakiza mechi mbili pekee kabla ya kufutwa kazi, huku akijiandaa kuiongoza timu hiyo dhidi ya Roma katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne.

Mustakabali wake umeendelea kuingiwa na mashaka baada ya United kupoteza mabao mawili bila kujibu dhidi ya Chelsea Jumamosi, matokeo yaliyoendeleza mwenendo wao mbaya wa kutoshinda mechi tisa mfululizo katika mashindano yote.

Carrick amesema hajui kitakachotokea baadaye, lakini hilo halijabadilisha maandalizi yake wala ari yake kuelekea mchezo dhidi ya Roma, licha ya matokeo mabaya ya hivi karibuni.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *