#Local News

WATAHINIWA WA KCSE WAANZA MITIHANI YAO

Watahiniwa wa kundi la pili kutoka mwisho kufanya mtihani wa KCSE wameanza mitihani ya maandishi, huku watahiniwa milioni moja elfu arobaini na nane mia tatu hamsini na watano wakitarajiwa kushiriki katika vituo zaidi ya elfu kumi.

Watahiniwa hao wameanza karatasi ya kwanza ya Kiingereza asubuhi, huku wanaosomea Kemia wakitarajiwa kufanya karatasi ya kwanza ya somo hilo alasiri.

Waziri wa Elimu Julius Ogamba amesema mitihani hiyo itaendelea hadi Ijumaa, Novemba 20, akihakikisha kuwa maafisa wa usalama na wasimamizi wa mitihani wako macho kuzuia udanganyifu na kulinda uadilifu wa zoezi hilo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *