WAKAZI WA RIRUTA WAHAMISHWA KUTOKA JENGO HATARI
Familia kadhaa katika eneo la Riruta Satellite jijini Nairobi zimeachwa bila makazi baada ya jengo la ghorofa kumi kando ya Barabara ya Kabiria kutangazwa kutokuwa salama kwa makazi.
Wakazi walilazimika kuhama kwa haraka baada ya idara ya usimamizi wa majanga ya serikali ya kaunti kubaini nyufa kubwa katika sehemu mbalimbali za jengo hilo na kutoa amri ya kutotumiwa.
Hali hiyo imewaacha wakazi wengi wakihangaika kutafuta mahali pa kulala, huku baadhi yao wakishindwa hata kuchukua mali zao za msingi kutokana na hofu ya jengo hilo kuporomoka.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































