WASHIRIKA WA RUTO WATANGAZA KAMPENI ZA 2027
Washirika wa serikali ya Rais William Ruto wameutaka upinzani kujiandaa kwa ushindani mkali katika uchaguzi wa 2027, wakieleza imani kuwa Rais atachaguliwa tena.
Wakizuru kaunti kadhaa nchini, Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi na Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya wamewahimiza Wakenya kuunga mkono ajenda ya maendeleo ya serikali
Viongozi hao wamesema serikali imejitolea kuhakikisha rasilimali za taifa zinagawanywa kwa usawa, wakitaka wananchi kuunga mkono juhudi hizo.
Imetayarishwa na cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































