#Local News

DCI YAFICHUA MTANDAO WA UDANGANYIFU KCSE

Maafisa wa upelelezi wamebaini mtandao wa udanganyifu katika mitihani ya KCSE unaodaiwa kufanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini, huku mshukiwa mkuu John Odhiambo Opiyo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kibabii, akitiwa mbaroni.

Maafisa hao wamepata simu ya mkononi inayodaiwa kutumika kusambaza mitihani, huku watahiniwa watatu wa KCSE kaunti ya Bomet wakifanya mitihani hospitalini, mmoja wao akijifungua Jumatatu asubuhi

Waziri wa Elimu Julius Ogamba amesema zaidi ya wanafunzi milioni moja wanafanya KCSE mwaka huu, idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *