GAKUYA APINGA KAULI YA KUMPISHA MGOMBEA MWINGINE NAIROBI
Mbunge wa Embakasi Kaskazini James Gakuya amesema vyama vya siasa vinapaswa kuruhusiwa kushiriki uchaguzi na kutoa uongozi, akisisitiza kuwa miungano lazima iwe na mifumo wazi ya kupata wagombea kwa haki.
Gakuya amesema hatakubali kuombwa kujiondoa ili kumpisha mgombea mwingine, akieleza kuwa hatua hiyo haiwezi kuleta umoja wa kweli ndani ya upinzani.
Ameutaka Muungano wa Upinzani kuweka utaratibu wa pamoja wa uteuzi wa wagombea wa ugavana, ili atakayechaguliwa kwa haki aungwe mkono na vyama vyote .
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































