#Athletics #Sports

CAROLINE NYAGA ALENGA KUFUZU MASHINDANO YA DUNIA

Bingwa wa Afrika wa mbio za mita elfu kumi mwaka 2022, Caroline Nyaga, analenga kushiriki kwa mara ya kwanza Mashindano ya Riadha ya Dunia, akilenga kufuzu kwa makala ya mwaka 2027 mjini Beijing, China

Nyaga mwenye umri wa miaka 33 hajawahi kuiwakilisha Kenya katika mashindano hayo, licha ya kutwaa dhahabu ya mita elfu kumi katika Mashindano ya Afrika nchini Mauritius kwa muda wa dakika 32 na sekunde 12

Mwanariadha huyo pia alitwaa shaba ya mita elfu tano katika mashindano hayo na fedha ya mita elfu moja mia tano mwaka 2024 nchini Cameroon, sasa akilenga kuendeleza mafanikio hayo katika jukwaa la dunia.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *