#Football #Sports

MCCARTHY AITAKA HARAMBEE STARS KUWAVURUGA AFRIKA KUSINI

Kocha wa Harambee Stars Benni McCarthy ameitaka timu yake kuonyesha ushindani mkali itakapokabiliana na nchi yake ya Afrika Kusini katika mechi mbili za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027, mwezi huu wa Novemba.

Kenya itacheza mechi ya kwanza ugenini Novemba 13 kabla ya kuikaribisha Bafana Bafana katika Uwanja wa Nyayo Novemba 17, kuanzia saa moja usiku, huku McCarthy akitarajia kuona kikosi chake kikikabiliana vilivyo na mojawapo ya timu zenye nguvu barani Afrika.

Ingawa Kenya tayari imefuzu kwa fainali za AFCON 2027 kama mwenyeji mwenza na Uganda na Tanzania, mechi hizo zitampa McCarthy nafasi ya kupima kikosi chake, baada ya kuanza kampeni za kundi D kwa sare ya bao moja dhidi ya Eritrea na kupoteza kwa bao moja dhidi ya Guinea.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *