WATAHINIWA WAWILI WA KCSE WAFARIKI KATIKA MATUKIO TOFAUTI
Nchi imeingia katika maombolezo kufuatia vifo vya watahiniwa wawili wa KCSE katika matukio tofauti, huku mitihani ya kitaifa ikiingia siku yake ya tatu .
Katika kaunti ya Homa Bay, Conjestina Achieng mwenye umri wa miaka 17 alifariki Jumatatu jioni baada ya kupata maumivu makali ya kifua, familia yake ikisema hali yake ilizorota muda mfupi baada ya kukamilisha karatasi ya pili ya mtihani.
Katika kaunti ya Siaya, Mwanafuzi mwenye umri wa miaka 18 alipatikana ameuawa nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Powo, huku kifo chake kikikatiza maisha yake wakati alipokuwa akianza mitihani yake ya kitaifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































