#Local News

KANJA AKANUSHA MADAI YA KUZUILIWA KWA TWAHA MWAIPAYA

Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja amekanusha madai kuwa mwanaharakati wa Tanzania Twaha Mwaipaya anazuiliwa katika kituo chochote cha polisi nchini Kenya.

Akifika mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Alexander, Kanja amesema hana taarifa kuhusu aliko mwanaharakati huyo wala iwapo yuko nchini Kenya.

Aidha, mkuu huyo wa polisi amekanusha kuhusika kwa maafisa wa polisi katika madai ya kutekwa nyara kwa Mwaipaya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *