GACHAGUA AWAKOSOA MUTURI NA MATIANG’I
Mivutano imeibuka ndani ya upinzani baada ya kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kuwajibu vikali kiongozi wa DP Justin Muturi na kiongozi wa Jubilee Fred Matiang’i kuhusu madai ya kuwadhulumu viongozi wenzake.
Gachagua amewakosoa baadhi ya viongozi wa upinzani kwa kile alichokitaja kuwa siasa za vikaoni, akiwatuhumu kwa kufanya mikutano hotelini badala ya kuwafikia wananchi mashinani.
Amesema kumwondoa Rais William Ruto mamlakani kutahitaji juhudi za pamoja na uhamasishaji wa wananchi mashinani, badala ya kutegemea mijadala na mivutano ya kisiasa pekee.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































