RISING LIONESSES ZAIANDIKIA KENYA HISTORIA
Timu ya raga ya wanawake ya Kenya, Rising Lionesses, imeandika historia baada ya kuilaza Australia alama 17 kwa 12 katika muda wa ziada na kutwaa medali ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar 2026 nchini Senegal
Ushindi huo umeipa Kenya medali yake ya kwanza ya dhahabu katika mashindano hayo, baada ya kuishinda Australia iliyokuwa miongoni mwa timu zilizotarajiwa kufanya vyema.
Rising Lionesses imehitimisha kampeni yake kwa mafanikio makubwa, ikionyesha moyo wa kupambana, kujituma na uwezo mkubwa wa kushambulia katika mashindano hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































