MANCHESTER UNITED YASITISHA KIPIGO CHA MECHI TISA
Manchester United imepata ushindi wa kusisimua wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Roma katika uwanja wa Old Trafford, baada ya kutoka nyuma kwa mabao mawili na kumpa kocha Michael Carrick nafuu kufuatia matokeo mabaya ya hivi karibuni
Roma ilianza kwa kasi na kupata mabao kupitia Matias Soule na Donyell Malen ndani ya dakika 20 za mwanzo, lakini Bruno Fernandes akaifungia United kupitia mkwaju wa penalti uliorudiwa baada ya kipa Devis Vasquez kuokoa jaribio la kwanza
Matheus Cunha alifunga mabao mawili, likiwemo la kusawazisha dakika saba kabla ya mchezo kukamilika na la ushindi dakika tatu baadaye, na hivyo kumaliza mfululizo wa United wa mechi tisa bila ushindi katika mashindano yote Katika Matokeo Mengine.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































