WINNIE ODINGA ASEMA ODM NI NYUMBANI KWAKE
Mwakilishi katika Bunge la Afrika Mashariki Winnie Odinga ambaye pia ni mwana wa hayati Raila Odinga amesema chama cha ODM ni nyumbani kwake baada ya kuidhinishwa na wawakilishi wa chama hicho katika Nairobi kuwa Naibu Kinara wa chama.
Odinga amesema kuwa Kaunti ya Nairobi ni muhimu katika uongozi wa chama hicho, akisisitiza kuwa lazima iwe na uwakilishi wake kutokana na mchango wake mkubwa katika kuimarisha chama hicho.
Ameongeza kuwa Nairobi imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa chama cha ODM kinasimama imara, hivyo kuhitaji nafasi ya uwakilishi katika ngazi za juu za uongozi wa chama.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































