OPERESHENI YA UOKOAJI EASTLEIGH YAINGIA SIKU YA 11
Operesheni ya kutafuta na kuokoa watu katika jengo lililoporomoka eneo la Eastleigh jijini Nairobi zinaendelea huku watu 11 wakiendelea kutajwa kuwa hawajulikani walipo.
Idadi hiyo ilipungua baada ya watu wanne waliodhaniwa kunasa kuthibitisha kuwa wako salama kwingineko, huku Mbunge wa Kamukunji Yusuf Hassan akieleza kusikitishwa na mwendo wa operesheni na kusema matumaini ya kupata manusura yamepungua.
Kwa upande wake, Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja amethibitisha kuwa jengo hilo lilikuwa likijengwa bila idhini stahiki za kisheria, akieleza pia changamoto katika mfumo wa haki ambapo baadhi ya wanaokiuka sheria huachiliwa baada ya kulipa faini ndogo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































